Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ZEC yawataka wananchi kujiandikisha kupiga kura

Muktasari:

  • Tume ya ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imewahamasisha wananchi kisiwani Unguja wajitokeze kujiandikisha katika siku tatu zilizopangwa kuanzia leo

Unguja. Wakati uandikishaji awamu kwanza ya wapigakura wapya ukianza leo Wilaya ya Kaskazini A Unguja, Mwenyekiti wa Tume ya ya uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji George Joseph Kazi amewataka wananchi ambao hawakuandikishwa leo wajitokeze tena kesho.

Uandikishwaji huo unatarajiwa kudumu kwa siku tatu, kuazia leo Desemba 23, 2023.

Akizungumza leo katika kituo cha kujiandikisha Shule ya Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A Unguja, Jaji Joseph amesema zipo changamoto wanazozipata baadhi ya wananchi walio na vitambulisho vipya hasa kutotambuliwa na mfumo.

"Kuna changamoto ambayo naamini maofisa wanazifanyia kazi na kesho watu hao wote wataandikishwa kwa kuwa taarifa zao tayari zitakuwa zinazoma kwenye mfumo," amesema JAJI Joseph.

Akizungumzia malalamiko ya baadhi ya wananchi kushindwa kuandikishwa kisiwani Pemba kwa kile walichoelezwa alama zao za vidole kutosoma, amesema changamoto hiyo inafanyiwa kazi kila inapojitokeza.

"Kuna watu kwa sababu ya harakati za kimaisha wamekuwa wakifanya kazi ngumu na kusababisha alama zao za vidole kutosoma kwenye mifumo, lakini wote wataandikishwa na kupata haki ya kupiga kura,” amesema Jaji Joseph.

Wakati hayo yakijiri, Mwananchi Digital imeshuhudia idadi ndogo ya uandikishaji katika vituo vya kujiandikisha kinyume na ilivyozoeleka katika chaguzi zilizopita.

Maryam Silima kutoka Mkwajuni amesema pamoja na idadi ndogo ya watu waliojitokeza kwa siku ya kwanza kwenye uandikishaji huo anaamini walio wengi huenda hawana taarifa.

Amesema bado wananchi wapo mitaani wakiendelea na shughuli zao za kila siku huku baadhi yao wakishindwa kujitokeza kwa sababu zao binafsi.

Naye Salim Abdalla kutoka Shehia ya Nungwi amesema kuna  vijana wameonyesha kukata tamaa na kuchoshwa, hivyo huamua kutokwenda kujiandikisha.

Pia, amasema inawezekana siku ya pili ya uandikishaji (kesho) watu watajitokeza kwa wingi kwa sababu watahamasishahana kupitia vyama vyao.