Miradi inayotekelezwa na Tanroads inaliunganisha jiji la Dar es Salaam kwa barabara nyingi zenye ubora

Muktasari:

Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam unahudumia jumla ya Kilomita 601.21 ambapo kati ya hizo kilomita 120.28 ni barabara kuu, kilomita 399.05 ni barabara za mikoa na kilomita 81.88 ni barabara za kukasimiwa. Kati ya hizo, km 385.13 ziko katika kiwango cha lami na km 216.08 ni changarawe.

 Sekta ya barabara ni sekta muhimu katika usafirishaji kwani inasafirisha takribani asilimia themanini (80%) ya wasafiri na zaidi ya asilimia tisini (90%) ya mizigo kote nchini.

Hivyo ukuaji wa uchumi hususan wa viwanda unategemea sekta hii katika usafirishaji wa malighafi kutoka kwenye maeneo ya uzalishaji hadi viwandani na pia usafirishaji wa bidhaa za viwandani hadi kwenye soko.

Ili sekta hii ichangie vizuri katika ukuaji wa uchumi ni lazima kuwe na mtandao wa barabara zinazopitika wakati wote wa majira ya mwaka, zilizo katika hali nzuri na zinazofikika sehemu zote muhimu za uzalishaji wa malighafi na masoko.

Dar es Salaam ikiwa ni moja ya majiji yanayokuwa kwa kasi barani Afrika katika shughuli za kiuchumi na kijamii ina mahitaji makubwa ya barabara zenye ubora ili kurahisisha shughuli hizo.

Ili kukidhi mahitaji hayo, Serikali kupitia Tanroads imekuwa ikijidhatiti kuhakik-isha Mkoa wa Dar es Salaam unaunganishwa na barabara za lami kwenye maeneo yote.

Kaimu Meneja wa Tanroads (M) Dar es Salaam, Mhandisi Ngusa Julius anaeleza namna Tanroadsilivyoweka mikakati katika kuhakikisha jiji hili linalokuwa kwa kasi linakuwa na barabara za kutosha na zenye ubora kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti hili ofisini kwake hivi karibuni.

Katika maelezo yake ya utangulizi, Mhandisi Julius anasema kuwa wakala wa barabara Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam unahudumia jumla ya Kilomita 601.21 ambapo kati ya hizo kilomita 120.28 ni barabara kuu, kilomita 399.05 ni barabara za mikoa na kilomita 81.88 ni barabara za kukasimiwa. Kati ya hizo, km 385.13 ziko katika kiwango cha lami na km 216.08 ni changarawe.

Serikali ya Awamu ya Tano imeweka nguvu katika uboreshaji wa sekta ya uchukuzi nchini. Je, Tanroads (M) Dar es Salaam inashiriki vipi katika juhudi hizi?

Mhandisi Julius anas-ema ofisi ya Tanroads Mkoa inashiriki kwa kiwango kikubwa katika usimamizi wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoani Dar es Salaam.

Miradi ya ujenzi na ukarabati wa mtandao wa barabara inayotekelezwa na Tanroads Dar es Salaam ni ipi?

Wakala unasimamia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam pamoja na miradi mingine mikubwa. Miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa ni kama ifuatayo:

Miradi mikubwa

Ujenzi wa barabara za juu eneo la Tazara (Mfugale Flyover) ambao umekamilika.

Mradi wa maboresho katika barabara ya Morogoro na Mandela (Ubungo) ambapo ujenzi wa Interchange unaendelea vizuri na kwa sasa umefikia zaidi ya asilimia 68.

Kwa sasa ujenzi wa madaraja ya barabara za kuelekea Mandela na Sam Nujoma unaendelea na unatarajiwa kukamilika Julai 22, 2020.

Mradi wa upanuzi wa barabara ya Bagamoyo kuto-ka Morocco mpaka Mwenge yenye urefu wa Kilomita 4.3 ambao utakamilika Februari 2021.

Mradi umefikia asilimia 28. Mradi wa ujenzi wa awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka (BRT ii) katika barabara za Kilwa, Bandari, Gerezani, Sokoine, Chang’ombe na Kawawa wenye urefu wa Kilomita 20.3 ambao ulianza Machi 1, 2019 na utakamilika Mei 5, 2022. Maendeleo ya mradi mpaka sasa ni asilimia 23.

 Upanuzi wa njia nane katika barabara ya Morogoro (Kimara-Kibaha), ujenzi wa mradi huu umefikia asilimia 67 na utakamilika Januari 20, 2021.

Mradi wa ujenzi wa daraja jipya la Salenda lenye urefu wa Kilomita 1.03 na barabara unganishi zenye urefu wa Kilomita 5.5. utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 21 na utakamilika Oktoba 14, 2021.

Mradi wa ujenzi wa daraja la Gerezani ambao umefikia asilimia 63 na utakamilika Disemba 2020,” anasema Mhandisi Julius.

Ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam

Serikali kupitia Wakala wa barabara Tanroads mwaka 2010 ilianza utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ili kutatua tatizo la msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Utekelezaji wa mradi huu ni kama ifuatavyo:

Mpaka kufikia Januari 2020 barabara ambazo ujenzi wake umekamilika

• Ubungo (Stendi ya mabasi) -Kigogo-kipita shoto (Round-about) na barabara ya Kawawa- Kilomita 6.4

• Kigogo Roundabout-Jangwani- Twiga Kilomita 2.72

• Jet Corner-Vituka-Davis Corner- Kilomita 10.3

• Ubungo Maziwa-Mabibo Exter-nal (Mandela) Kilomita 0.65

• Tabata Dampo-Kigogo Kilomita 1.6

• Mbezi mwisho-Marambamawili-Kifuru-Kinyerezi- Banana sehemu ya Kifuru mpaka Kinyerezi Kilomita 14.

• Tegeta Kibaoni-Wazo Hill-Goba- Mbezi/Morogoro Road sehemu ya Madale mpaka Mbezi Mwisho/Goba Kilomita 12.

• Tanki Bovu samaki wabichi- Goba Kilomita 9.

• Kimara Baruti-Msewe Kilomita 2.6. • Kimara-Kilungule-External (Mabibo Mandela) Kilomita 3.

• Ujenzi wa daraja la Mlalakuwa katika barabara ya Mwai Kibaki.

• Mradi wa ujenzi wa daraja la Kinyerezi katika barabara ya Banana-Segerea.

Barabara ambazo ujenzi wake unaendelea

• Banana-Kitunda-Kivule-Msongola sehemu ya Kitunda-Kivule Kilomita 3.2 umeanza tarehe 1 Oktoba 2019 na utakamilika tarehe 30 Septemba 2020. Mpaka sasa utekelezaji umefikia asilimia 25.

• Tungi-Kibada Kilomita 3.8. Ujenzi umeanza tarehe 1 Januari 2019 na utakamilika tarehe 27 Machi 2020. Utekelezaji ni asilimia 70.

• Ardhi-Makongo-Goba Kilomita 9. Ujenzi umekamilika Kilomita 4 na sehemu ya Makongo Juu mpaka Chuo cha Ardhi (Km 4.5) ujenzi unaendelea. Kazi ya ujenzi itakamilika Oktoba 31, 2020 Ujenzi umefikia asilimia 5.

• Tegeta Kibaoni-Wazo Hill-Goba sehemu ya Madale mpaka Wazo Hill (km 6) umeanza Novemba 1 2019 na utakamilika baada ya miezi 18. Utekelezaji kwa sasa ni asilimia 5.

Barabara ambazo usanifu umekamilika na ujenzi unatarajiwa kuanza

• Kibada-Mwasonga-Tundwisongani-Kimbiji Kilomita 41.

• Mjimwema-Kimbiji-Pembamnazi, Kilomita 30

Barabara ambazo usanifu unaendelea

• Mbagala Rangitatu-Kongowe Kilomita 3.8 ili ipanuliwe njia mbili na kuwa nne.

• Kimara-Bonyokwa-Kinyerezi Kilomita 8 kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami

• Temboni/Morogoro Road- Goba Kilomita 6.99 kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami.

• Makutano ya barabara katika maeneo ya Magomeni-Moroc-co-Palm Beach-Mwenge- Salenda-Fire-Tabata na Buguruni kwa ajili ya ujenzi wa madaraja ya juu,” anasema Mhandisi Julius.

Miradi ya matengenezo ya kawaida ya barabara

Anasema, pia Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam inasimamia maten-genezo ya kawaida ya barabara ili kuzifanya zipitike majira yote ya mwaka. Miradi ya matengenezo ya kawaida inayotekelezwa ni; kuziba mashimo, kusafisha mitaro, kuten-geneza sehemu korofi, kufyeka nyasi na matengenezo ya taa za barabarani.

Mafanikio ambayo Tanroads, Dar es Salaam inajivunia

“Ofisi ya Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam inajivunia kushirikishwa katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya barabara kama taasisi ya Serikali ambapo barabara nyingi zimejen-gwa kwa kiwango cha hali ya juu. Miradi hiyo ni kama barabara za kuondoa msongamano jijini Dar es Salaam na miradi mikubwa ambayo ina manufaa kwa jiji na taifa kwa ujumla,” anasema Mhandisi Julius.

Ni changamoto gani mnakutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yenu?

“Wakala wa barabara Mkoa wa Dar es Salaam katika utekelezaji wa majukumu yake umekuwa ukikabiliana na changamoto mbalimbali. Baadhi ya changamoto hizo ni:

Kuvamiwa kwa maeneo ya hifadhi ya barabara

Njia za watembea kwa miguu pamoja na hifadhi ya barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam zimevami-wa na wafanyabiashara ndogondogo kinyume cha sheria na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara.

Maeneo ambayo wafanyabiashara wameanzisha masoko kinyume cha sheria ni; Mwenge, Ubungo, Ukonga, Mombasa, Gongo la Mbo-to, Chanika, Mbagala Rangi Tatu, Tegeta, Bunju A, Bunju B, Kongowe, Kimara Mwisho, Mbezi Luis, (Mbezi Mwisho), barabara ya Uhuru katika maeneo ya Buguruni sokoni, Ilala Boma mpaka Lumumba, barabara ya Mabibo-Urafiki na Mbande.

Utupwaji holela wa taka katika mifereji ya maji

Utupaji holela wa taka katika mitaro ya maji na pembezoni mwa barabara umekuwa ukisababisha kuziba kwa mitaro ya maji na hivyo kusababisha mafuriko ya maji barabarani hasa maeneo yaliyo na wafanyabiashara ndogondogo.

Uharibifu wa miundombinu

Taa za barabarani na za kuongozea magari pamoja na alama za barabarani zimekuwa zikigongwa katika maeneo mbalimbali. Pia matukio ya wizi wa nyaya za umeme (armored cables) zinazowasha taa za barabarani yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku,” anas-ema Mhandisi Julius.

Ni wito gani mnatoa kwa Watanzania?

“Ofisi ya Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam inatoa wito kwa wananchi kufuata sheria namba 13 ya mwaka 2007 na kanuni zake za mwaka 2009 kwa kufanya biashara, kujenga katika hifadhi ya barabara. Kufanya hivyo kutarahisisha utekelezaji wa majukumu ya Wakala kwa kuwa wao ni wadau namba moja katika kutunza miundombinu ya barabara na madaraja,” anasema Mhandisi Julius.