NVC, Zoetis na A.L.P.H.A katika dhamira moja ya kukuza sekta ya mifugo nchini

Muktasari:

Nasimz Veterinary Care (NVC) ni watoa huduma mbalimbali za mifugo wanaopatikana jijini Mwanza, (Magharibi mwa Tanzania). Kampuni hii ilianzishwa Oktoba 12, 2017 lakini ilianza kufanya shughuli zake kamili Agosti 2018 wakitoa huduma za mifugo kwa Kanda ya Ziwa

Sekta ya mifugo ina mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi nyingi za Kiafrika. Hata hivyo, nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara licha ya kuongoza kuwa na mifugo mingi bado zinakabiliwa na changamoto ya magonjwa ya mifugo.

Wafugaji wengi katika nchi hizi hawana elimu sahihi juu ya uboreshaji wa afya za mifugo na hivyo kusababisha tatizo la usalama wa chakula.

Hivyo, kwa sababu hii, Nasimz Veterinary Care (NVC) ikishirikiana na Zoetis na A.L.P.H.A iliamua kujitoa kwa asilimia zote kuboresha afya za wanyama kwa kutoa huduma kadhaa za kitabibu hapa nchini. Mkurugenzi wa NVC, Rahim Jivraj anaelezea kwa ufupi kuhusiana na shu-ghuli za kliniki hiyo.

“Nasimz Veterinary Care (NVC) ni watoa huduma mbalimbali za mifugo wanaopatikana jijini Mwanza, (Magharibi mwa Tanzania). Kampuni hii ilianzishwa Oktoba 12, 2017 lakini ilianza kufanya shughuli zake kamili Agosti 2018 wakitoa huduma za mifugo kwa Kanda ya Ziwa,” anasema Jivraj na kuongeza

“Ikiwa imejikita katika utunzaji maalum wa wanyama wadogo wa nyumbani na mifugo, kampuni hii inatoa huduma za chanjo na kinga kwa wanyama, uchunguzi na matibabu. Kampuni hii ina wataalam wa hadhi ya juu wa kutoa huduma bora.” Jivraj anasema, bidhaa na huduma zinazotolewa ni pamoja na:

• Vipimo vya kitabibu,

• Upasuaji,

• Uchunguzi wa kimaabara,

• Huduma za chanjo,

• Ufafanuzi wa ripoti baada ya kifo,

• Ugawaji wa dawa za wanyama na

• Usimamizi wa wanyama/ushauri wa elimu.

Timu ya wafanyakazi

Jivraj anasema kuwa, “Timu yetu inajumuisha daktari mmoja wa upasuaji wa mifugo, wasaidizi wa kitabibu watatu, mtaalamu wa ukuzaji wanyama na ofisa elimu wa jamii.”Upanuzi na ukuaji “Kampuni yetu inatoa huduma za kubeba wagonjwa, nyumba hadi nyumba, na huduma za wagonjwa wanaokwenda kutibiwa na kuondoka na wale wanaolazwa katika kliniki iliyopo Isamilo Mwanza.

“Pia kuna vifaa vya kutolea huduma za wanyama vinavyohamishika na zana za uchunguzi wa magonjwa zinazofanya uchanganuzi katika eneo husika vipo kwa ajili ya kuwahudumia wateja popote walipo,” anabainisha Jivraj.

Anaongeza kuwa, “Kwa wanyama wadogo wa majumbani, kituo cha kliniki cha kampuni hiyo hutoa huduma za matibabu kwa wanyama wanaopelekwa na kuondoka na wale wanaolazwa, na huduma za uchunguzi wa maabara. Sisi pia tunatoa program za mafunzo katika jamii husika ambapo mwakilishi wetu huelimisha na hutoa huduma za ushauri wa usimamizi wa wanyama.

Mkakati wa kampuni hii ni kuwa na kituo cha kutolea huduma za kitabibu za wanyama katikati ya jiji ambacho kitaweza kutoa huduma za uchunguzi wa maabara, dawa na malisho.” Fursa za kuboresha afya na uzalishaji wa mifugo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Jivraj anasema, kulingana na Umoja wa Mataifa (UN) idadi ya watu ulimwen-guni inatarajiwa kuongezeka takriban watu bilioni 2 na kufikia bilioni 9.7 ifikapo mwaka 2050. Ongezeko hilo, sambamba na ukuaji wa viwango vya umiliki mali, linalosababisha kuibuka kwa tabaka la kati ulimwenguni, limesababisha kuongezeka kwa mahitaji ya chakula.

Jambo hili linaleta changamoto na fursa kwa pamoja kwa wadau waliopo katika sekta ya kilimo biashara. “Mfumo endelevu na fanisi wa kilimo una tija kwa shughuli zinazoendesha maisha ya watu na uchumi wa Tanzania.

Uwekezaji katika upatikanaji wa bidhaa na huduma muhimu za mifugo na miundombinu ya kutosha inayohitajika kwa matibabu ya wanyama, huwa na athari chanya za muda mrefu,” anasema Jivraj.

Kuongezeka kwa upatikanaji elimu ya afya ya wanyamaMkuu wa Mpango wa A.L.P.H.A, Zoetis, Tetiana Miroshnychenko anasema; “Ongezeko la idadi ya watu ndiyo chanzo kikubwa cha kuwepo kwa mpango wa Zoetis African Livestock Productivity and Health Advancement (A.L.P.H.A.) ulioanzishwa na Taasisi ya Bill na Melinda Gates (Bill and Melinda Gates Foundation) ambao una lengo la kuboresha afya za mifugo na kuleta athari chanya kwa shughuli za wakulima kwa nchi za Tanzania, Nigeria, Ethiopia na Uganda.”

Miroshnychenko anaongeza kuwa, “Nchi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara zinafahamika kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo duniani na idadi kubwa ya wafugaji ambao wamo katika lindi kubwa la umaskini. Uboreshaji afya na uzalishaji ni muhimu kwa ajili ya usalama wa chakula kwenye maeneo yenye wanyama wengi na changamoto za magonjwa ya binadamu, kwa kuwa na athari ya moja kwa moja katika kilimo biashara duniani kote kutokana na kutochunguzwa kwa milipuko ya magonjwa kama vile homa ya nguruwe au mafua ya Avian.”

Kuboresha uwezo wa utambuzi wa magonjwa na miundombinuMiroshnychenko anafafanua kuwa, mpango wa A.L.P.H.A unatoa zaidi mafunzo. Katika kuhakikisha kunakuwepo kwa faida endelevu na za muda mrefu, unasaidia pia kuboresha miundom-binu ya afya ya mwili ya wanyama.

Kwa mfano; ushirikiano wenye mafanikio na wadau wa biashara za maabara umesaid-ia kwa kiasi kikubwa kutengenezwa kwa maabara imara za kufanyia uchunguzi wa magonjwa katika nchi wanachama wa mpango wa A.L.P.H.A.Mpango huu unasaidia maabara ya utambuzi wa magonjwa za umma na binafsi, hapa nchini A.L.P.H.A imeshirikiana na Silverlands kule Iringa, Nasimz ya Mwanza, Interchik jijini Dar es Salaam, na hivi karibuni ushirikiano wetu utaongeza wigo kwa vyuo vikuu viwili vilivyojijengea heshima, vyuo vya Nelson Mandela na Sokoine.

“Ushirikiano huu husaidia kuanzisha vituo vipya au kukuza vilivyopo, lakini pia inazingatia kuelimisha wanasayansi wa maabara ndani ya nchi ili waweze kutumia teknolojia ya utambuzi wa magonjwa ya kisasa. Maabara mpya zitatoa huduma za uchunguzi wa magonjwa kwa kutumia teknolojia ya ELISA na awamu ya kwanza itajikita na vipimo vya utambuzi wa magonjwa ya kuku kama vile ugonjwa wa Newcastle, virusi vya anemia vya kuku, virusi vya maambukizi ya bronchitis, virusi vya Reo, Mycoplasma gallisepticum, virusi vya mafua ya Airl na virus vya ugonjwa wa bursal,” anasema Miroshnychenko.

Miroshnychenko anasema, “Awamu ya pili, itajikita na vijidudu na kada ya uchunguzi wa vimelea vya damu vya ndani (Trypanomosiasis, East Coast Fever, Anaplasmosis, Babesiosis, Helminthiasis), upimaji na uthibitisho wa Brucellosis na Kifua kikuu cha Bovine, na utumiaji wa ultrasound kugundua ujauzito.”

“Maabara hizi kwa kushirikiana na Zoetis hutengeneza mtandao wa waku-lima na wataalam wa mifugo, ambao tayari wanaweza kutumia application ya LabCards, ambayo inasaidia kufuatilia sampuli na mtiririko wa mawasiliano. A.L.P.H.A. itaendelea kutoa msaada muhimu katika njia ya mafunzo ya hali ya juu, wafanyakazi, na ufikiaji wa maarifa na utaalam wa kimataifa,” anaongeza.

Kuongezeka kwa upatikanaji wa bidhaa za kisasa

Mwakilishi wa A.L.P.H.A, Tanzania, Bryan Kelly anasema, “Zoetis itakusanya taarifa muhimu kwa ajili ya usajili wa bidhaa za afya, njia mpya za utambuzi wa magonjwa na chanjo nchini, kama sehemu ya mpango huo. Mara tu taratibu zitakapoidhinishwa, zitasaidia kutoa wigo mpana wa suluhisho la kukinga magonjwa na matibabu katika mifugo. Hivi sasa, idadi ndogo ya bidhaa zinapa-tikana nchini kwa kutegemea vibali vya uagizaji kupitishwa kama inavyotakiwa.”

“Bidhaa hizo zinasambazwa na msambazaji aliyeidhinishwa na Zoetis anayefahamika kama S&J Animal Tech kwa kuzingatia kwa ukamilifu mchakato wa ufuatiliaji wa mnyororo kutoka hatua ya uzalishaji hadi mtumiaji wa mwisho kupitia vifaa vya ukaguzi wa taarifa. Vifaa hivi vimeundwa kufuatilia na kuripoti mabadiliko ya joto kwa bidhaa zinazosafirishwa.A.L.P.H.A inafanya kazi kwa bidii kuhakikisha mafunzo na utaalam una-tolewa kwa washikadau wote juu ya utunzaji wa bidhaa na ufuatiliaji wa mnyororo wa thamani, ambao bado ni changamoto kubwa katika mazingira ya Tanzania,” anasema Bryan Kelly.

Kuwawezesha wataalamu

Bryan Kelly anasema; “Uwezeshaji wa sekta ya mifugo ni nyenzo muhimu ya A.L.P.H.A. Wataalam wa mifugo mara nyingi hawaonekani muhimu mbele ya wakulima ambao hushindwa kupata huduma nzuri kutoka kwao. Zoetis imefanya mafunzo ya kidigitali tofauti kupitia VetVance na maktaba ya marejeo ya wataalamu wa mifugo, inayoitwa Vetlexicon Bovis kwenye jukwaa linaloitwa Learn & Grow, kwa kuongeza, wataalam wa mifugo wa Zoetis huendesha mafunzo ya kiufundi ya watoa huduma za mifugo na wasambazaji ili kusaidia ukuaji wa taaluma hiyo.”

Bryan Kelly anasisitiza kuwa, Zoetis na A.L.P.H.A, wanafanya kazi karibu na Baraza la Mifugo la Tanzania (VCT) katika kuzindua na kukuza “Tovuti ya Learn and Grow” kwa wataalamu mbalimbali nchini.

Kufungua fursa endelevu

“Uendelevu ni msingi wa shughuli zetu za utoaji misaada, na kwa hivyo tunaona ufadhili kutoka taasisi ya Gates kama ‘nyongeza’ ya kuinua shughuli zetu za zamani na washirika wetu wote waliopo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Inaturahisishia sisi kusaidia washirika katika kutengeneza moduli za mafunzo, huduma, njia za utambuzi wa magon-jwa na jalada la bidhaa ili kufanikisha kwa miaka ijayo bila kutegemea ufadhili zaidi,” anaongeza Bryan Kelly.

 “Tukiwa kama kampuni inayoongoza inayohusika na afya ya wanyama ulimwenguni, tunaamini kwamba tuna uwezo wa kukabiliana na changamoto hii. Uwekezaji wetu katika shughuli maalum kusaidia jamii za ufugaji na kilimo, zilizotolewa kwa kushirikiana na wadau wa ndani zitasaidia kufungua mlango wa uwepo wa vituo bora na mbinu za kitabibu, pamoja na fursa ya kuongezeka kwa uwekezaji kutoka sekta ya kilimo.”