Marekani yasikitishwa na tamko la ZEC kufuta uchaguzi Z’bar

Wednesday October 28 2015

 

By Matilda Tarimo,Mwananchi Digital

Dar es Salaam. Serikali ya Marekani imesema imestushwa na tamko lililotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ambapo ametamka kusudio lake la kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa Zanzibar.

Taarifa ya Ubalozi wa Marekani nchini iliyotumwa kwa vyombo vya habari inasema hatua hiyo inasitisha mchakato wa uchaguzi uliofanyika vizuri na kwa Amani.

“Tunatoa wito wa kuondolewa kwa tamko hilo  na kuzisihi pande zote kudhamiria kwa dhati kuukamilisha mchakato huu wa kidemokrasia kwa uwazi na kwa Amani,” inasema taarifa hiyo.