#WC2018 Afrika macho yote kwa Mane, Salah leo

Moscow, Russia. Matumaini ya Afrika kufanya vizuri katika Kombe la Dunia itaamuliwa leo wakati washambuliaji wake wawili nyota Mohamed Salah na Sadio Mane watakaposhuka uwanjani kwa mara ya kwanza.

Washambuliaji hao wa Liverpool, Salah na Mane wanategewa kufuata nyayo za nyota wa Tunisia, Ferjan Sassi aliyefunga bao la kwanza kwa Afrika jana wakati nchi yake kilala kwa mabao 2-1 kwa England.

Salah anayesumbuliwa na tatizo la bega leo atalazimika kuiongoza Misri dhidi ya wenyeji Russia katika mchezo ambao utaamua hatma ya mabingwa hao mara saba wa Afrika.

Katika mchezo wa kwanza ambao Misri ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Uruguay, mshambuliaji Salah alikuwa benchi akishudia.

Hivyo ni lazima Misri ipate ushindi dhidi ya Russia ili kufufua matumaini yake ya kubaki Kombe la Dunia ila kufungwa au sare itawaweka pabaya.

Senegali itakuwa ikicheza mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia tangu 2002, huku matumaini yao yote yakiwa kwa Mane dhidi ya Poland leo katika mchezo wa Kundi H.

Kocha wa Senegal, Aliou Cisse aliyekuwa nahodha wa nchi hiyo 2002 timu hiyo ikifuzu kwa robo fainali kwa mara ya kwanza, pia waliwafunga mabingwa watetezi Ufaransa katika mechi ya kwanza ya hatua ya makundi.

"Mane ni mchezaji wa tofauti uwezi kumlinganisha na mchezaji mwingine wa Senegal. Anauwezo wa kubadilisha matokeo wakati wowote," alisema Cisse mwenye miaka 42.

Mane amefunga mabao 33, katika misimu miwili tangu alipojiunga Anfield kwa gharama ya pauni 34milioni akitokea Southampton.

Mechi za Leo Juni 19

Kundi H

Colombia v Japan (Saa 9:00 Alasiri)

Poland v Senegal (Saa 12:00 Jioni)

Kundi A

Russia v Misri (Saa 3:00 Usiku