Aliyemng’oa Wenger, akimbia lawama Arsenal

Muktasari:

  • Gazidis aliyesimamia mpango wa kuondoka kwa Arsene Wenger ndani ya Arsenal alitumikia klabu hiyo kwa miaka kumi na moja ya kazi ngumu aliyoifanya ni kuilainisha bodi ya klabu hiyo hadi kumuondoa Wenger na kumuajiri Unai Emery, kuwa kocha mpya.

London, England. Bila shaka mambo yamebadilika kabisa ndani ya Arsenal, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo Ivan Gazidis, ni kama amekimbia lawama kwa kuondoka na kujiunga na AC Milan ya Italia.

Gazidis aliyesimamia mpango wa kuondoka kwa Arsene Wenger ndani ya Arsenal alitumikia klabu hiyo kwa miaka kumi na moja ya kazi ngumu aliyoifanya ni kuilainisha bodi ya klabu hiyo hadi kumuondoa Wenger na kumuajiri Unai Emery, kuwa kocha mpya.

Hata hivyo Gazidis hajaiacha Arsenal vibaya kwani alifanikisha kwanza ujio wa mrithi wake Raul Sanllehi aliyekuwa mtndaji wa Barcelona ambaye sasa anakuwa mkuu wa michezo.

Taarifa ya klabu iliyotolewa jana ilisema kuwa Sanllehi atakuwa mkuu wa masuala yote yahusuyo  soka ndani ya klabu hiyo na anatarajiwa kuiletea mafanikio kama alivyofanya akiwa Barcelona.

Mbakli ya Raul Sanllehi Arsenal pia imemrejesha mtaalamu wa uchumi Vinai Venkatesham ambaye sasa atasimamia masuala yote ya kiuchumi na utawala ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake Emirates, akiwa ndiye Mkurugenzi Mtendaji.

Uteuzi wa watendaji hao wapya uliweka kwenye mtandao wa klabu ya Arsenal, mapema leo asubuhi pamoja na mtandao wao wa kijamii wa Twitter.

Venkatesham mbali ya kufanya kazi na Arsenal miaka ya nyuma aliwahi kuwa Mkurugenzi wa uchumi kwenye kamati ya michezo ya Olimpiki ya ‘London 2012 Olympic’.