Chelsea yamtaka nyota wa Man City

Muktasari:

  • shambuliaji huyo wa zamani wa Man City amerudi katika ubora wake tangu alipotua Italia

 Klabu ya Chelsea inatarajiwa kufanya usajili wa kushangaza kwa kumsajili mshambuliaji wa AS Roma Edin Dzeko.

Dzeko aliwahi kuitumikia Manchester City kabla ya kwenda kungara katika Ligi Kuu Italia ‘Seria A’ na kocha Mtaliano Antonio Conte amevutiwa na kipaji chake.

Conte amepanga kumtoa kwa mkopo mshambuliaji Michy Batshuayi kwenda AS Roma ili kutoa fursa kwa Dzeko kujiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu England.

Kocha huyo huenda akaibua mjadala mwingine, baada ya juzi kudai anataka kumsajili mshambuliaji wa West Ham United Andy Carroll ambaye amewekwa sokoni kwa Pauni20 milioni.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa England ameshindwa kutamba msimu huu kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara.