De Gea ayakubali mavitu ya Arrizabalaga

Muktasari:

Kipa huyo amekuwa mmoja wa makipa hodari Ulaya, amekuwa akiwindwa kwa nguvu zote na Real Madrid na Arsenal katika miezi ya karibuni.

Kipa wa Manchester United, David De Gea anaamini mchezaji mwenzake, Kepa Arrizabalaga atakuwa mchezaji mkali lakini akiendelea kubakia katika klabu yake ya Athletic Bilbao.

Kipa huyo amekuwa mmoja wa makipa hodari Ulaya, amekuwa akiwindwa kwa nguvu zote na Real Madrid na Arsenal katika miezi ya karibuni.

De Gea anaamini Arrizabalaga anaweza kuwa mbele zaidi kama atajituma na kwa mazoezi anayofanya yatamfikisha mbali zaidi.

Kipa huyo wa Manchester United alisajiliwa kutoka klabu ya La Liga, Atletico Madrid mwaka 2011, lakini akasema kubakia nyumbani kwa Arrizabalaga, kutambeba zaidi.

æWachezaji walioondoka Hispania kama mimi De Gea said ni ngumu kwa mashabiki kuwafuatilia, kama mtu akicheza nyumbani, ni rahisi kufuatiliwa na mashabiki na wakaonekana.

 

æKimsingi, ndiyo maana ninataka kurudi nyumbani. æKepa bado ni mdogo na umri unamruhusu. kama ukifanya naye mazoezi, unaona kabisa huyu ana uwezo wa kufika mbali."

 

Arrizabalaga alianza kuichezea Athletic Bilbao mwaka 2015 na ametajwa kuwa anataka kujiunga na Real Madrid usajili wa Januari.