Saturday, November 11, 2017

Hazard: Itakuwa ni ndoto kucheza chini Zidane

 

Kiungo Eden Hazard amekiri kuwa kucheza chini ya kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ndiyo lengo lake katika siku za usoni.

Winga huyo wa Chelsea amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Santiago Bernabeu kila wakati, tangu akiwa na Lille.

Japokuwa kwa sasa hafikiri kuhusu uhamisho huo, lakini Hazard amekiri kuwa ndoto yake kucheza chini ya mtu anayemvutia zaidi tangu utoto wake.

"Kila mtu anajua heshima niliyokuwa nayo kwa Zidane kama mchezaji, pia kama kocha ni mtu ninayemvutia," aliimbia RTL.

"Sijui nini kitatokea katika maisha yangu ya soka ya baadaye, lakini itakuwa ni ndoto yangu kucheza chini ya Zidane.

"Lakini kwa sasa nafurahi maisha yangu Chelsea. Bado kuna mambo natakiwa kupata nikiwa hapa akili yangu yote ipo kama mchezaji wa Chelsea."

 

-->