Bondia Anthony Joshua alazimisha kupanda ulingoni

Muktasari:

Bondia Joshua alazimisha kupata pambano ili kutafuta fedha lakini hatakiwi kupigana kwa sasa.

Marekani. Promota Eddie Hearn amesema kwamba bondia Anthony Joshua anakaribia kuthibitisha pambano lake dhidi ya Joseph Parker.

Hata hivyo, pambano hilo sio la kuwania mkanda wowote kutokana na Joshua kutoruhusiwa kupigania mkanda wowote

Hivi karibuni Chama cha Ngumi Marekani kilimtahadharisha Joshua kutojihusisha na pambano lolote na kama atafanya hivyo uongozi wa chama hicho hautambui na hautawajibika kwa lolote.