Lukaku ajipeleka Andelecht

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo katika msimu huu amekuwa na kiwango kisichotabilika ndani ya Man United

Mshambuliaji Romelu Lukaku ameahidi atarudi tena kuichezea Andelecht mara tu maisha yake ya Manchester United yatakapofika ukingoni.

Fowadi huyo aliyenaswa na Man United kwa ada ya Pauni 75 milioni mwaka jana, ameshafunga mabao 19 katika kikosi hicho ambacho maisha yake yamekuwa ya kupanda na kushuka.

Lukaku ametengeneza jina lake kuwa kubwa huko England kutokana na mabao yake aliyokuwa akifunga Everton, lakini soka lake la kulipwa alianzia kulicheza huko Ubelgiji kwenye klabu ya Anderlecht, ambako mechi yake ya kwanza ilikuwa mwaka 2009 kabla ya kunaswa na Chelsea wakati akiwa na umri wa miaka 18.

“Ndoto zangu siku zote ni kuichezea Anderlecht,” alisema Lukaku.

“Kabla sijaachana na maisha ya soka kama mchezaji, nitarudi kuichezea timu hiyo, naweza kutoa ahadi hiyo. Nilikuwa na nyakati nzuri sana kule.”

Lukaku anaamini Man United bado wapo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England licha ya kocha wao, Jose Mourinho kusisitiza mambo yamewashinda.