Lwandamina apigwa butwaa Yanga kutimuliwa Uwanja wa Taifa

Muktasari:

Yanga itacheza na St  Louis mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

KOCHA mkuu wa Yanga, George Lwandamina ameshangaa kitendo cha klabu yake kugomewa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa na kuwaruhusu wapinzani wao St Louis ya Shelisheli kuutumia.

Lwandamina amesema, anashangaa kuona Yanga ambao ni wenyeji wanagomewa kufanya mazoezi kwenye uwanja huo wakati wageni wanaruhusiwa, jambo ambalo ni kinyume na mataifa mengine ambayo huwapa kipaumbele wenyeji na kuwafanyia 'figisu' yaani mazingira magumu kwa wageni.

"Hawataki timu ifanye mazoezi Uwanja wa Taifa zaidi ya kucheza tu siku ile ya mechi, wakati wapinzani wetu wameruhusiwa kweli hii ni sawa?," alihoji Lwandamina ambaye kwa kipindi hiki kikosi chake kinafanya mazoezi Uwanja wa Polisi.

Yanga itacheza na St  Louis mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.