Thursday, June 14, 2018

SportPesa, Airtel yazindua promosheni kwa mashabiki Simba na Yanga

 

By Majuto Omary

Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na SportPesa imezindua promosheni ya mwezi mmoja ijulikanayo kama Amsha Amsha  na  Airtel Money na ushinde ambapo wateja wa Airtel watajishidia zawadi kabambe pale wanapobet kwa kutumia Airtel Money.

Promosheni hiyo ya Airtel Shinda na SportPesa ambayo imeanza leo na itakamilika Julai 15.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania, Isack Nchunda amesema promosheni hiyo inatoa nafasi nyingine kwa wateja kuweza kujishindia zawadi kabambe kwa kubet wakitumia Airtel Money na kushinda zawadi mbalimbali kama king'amuzi, simu za mkononi pamoja na  jezi za Yanga na Simba.

Nchunda amesema promosheni itaanza saa sita usiku na itaendelea kwa muda wote wa promosheni ambao ni mwezi mmoja.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti  SportPesa, Tarimba Abbas alisema kuwa  wameamua kuungana na kampuni ya Airtel kwa lengo la kupanua wigo zaidi kwa wadau wao.

Tarimba amesema kuwa wanatarajia kuona mashabiki wengi wa Yanga na Simba wanashiriki katika promosheni hii kwa lengo la kujishindia zawadi mbalimbali pamoja tiketi za kuona mechi za Yanga na Simba.

Alisema kuwa zawadi za washindi zitakuwa zikitolewa kwa kila wiki na kuwaomba wadau wa soka kujitokeza katika promosheni hiyo.

-->