Mazoezi ya Simba yawatikisa Nkana

Nyota wa Simba walifanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Nkana Rangers ambao watautumia kwa ajili ya mechi ya kesho.

Wachezaji wa Simba walianza mazoezi ya viungo ambayo yalikuwa yakisimamiwa na kocha wa viungo Adel Zrane.

Banda ya kumaliza mazoezi ya viungo walianza kufanya yale ya kupasiana kupiga mipira mirefu.

Baada ya kumaliza mazoezi ya kupiga mipira mirefu kocha mkuu Patrick Aussems alisimamia mazoezi ya kucheza nusu uwanja huku akiwagawa makundi mawili.

Aussems alionekana anataka wachezaji wapige pasi fupi kwa haraka na alikuwa hataki kuona mchezaji anakaa na mpira kwa muda mrefu.

Walipo maliza mazoezi hayo walifanya mazoezi ya kupiga mashuti na waliokuwa wakifanya zoezi hili ni washambuliaji tu.

Simba walifanya mazoezi hayo mepesi kwa muda wa saa moja kwani walianza saa 9:00 na kumaliza 10:00 jioni kwa saa za hapa Zambia.