Bondia Mtanzania amvuruga Mzungu kwa makonde

Muktasari:

  • Asema kilichomuangusha kwenye pambano lake dhidi ya Andrejs Podusovs nchini Latvia  ni kucheza kwake ugenini.

 Bondia wa ngumi za kulipwa Idd Mkwela wa uzani wa  Lightweght amesema kilichomuangusha kwenye pambano lake dhidi ya Andrejs Podusovs nchini Latvia  ni kucheza kwake ugenini.

Mkwela alipoteza pambano hilo la  kuwania Ubingwa wa Dunia wa International  Boxing Association (IBA)  Jumamosi ya Machi 17 kwa pointi za majaji wa 2-1.

“Nilicheza vizuri lakini naona labla kwa sababu nilikuwa ugenini ndiyo imekuwa sababu ya kumpa mpinzani wangu huo ubingwa,kwa kawaida pale ambapo unampiga mtu na akatokwa na damu huwa ni TKO lakini haikuwa hivyo.

“Nilimpiga na alitokwa na damu usoni, kuna muda hadi pambano lilisimamishwa ili ulingo ufanyiwe usafi kutokana na damu, nimesikitishwa sana ila sikuwa na namna nyingine ya kufanya,” alisema Mkwela.

Pambano hilo ambalo amepoteza Mkwela limekuwa pambano lake la kwanza kwenye uchezaji wake masumbwi ya kulipwa, bondia huyo.

Kupigwa kwa Mkwela kumemuwekea doa kwenye rekodi yake kwa kuwa pambano  wake wa kwanza kupoteza kwenye ngumu hizo za kulipwa, kiujumla bondia huyo amecheza jumla ya mapambano nane na ameshinda mara  saba.