Kuumia kwa Morata pengo Chelsea

Muktasari:

  • Antonio Conte yupo katika wakati mgumu baada ya kuthibishwa kuwa kinara wake wa ufungaji kuwa njea hivyo kubaki na Michy Batshuayi katika safu yake ya ushambuliaji

CHELSEA imepata pigo kubwa  baada ya kufahamia kuwa Alvaro Morata atakuwa nje kwa wiki sita kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Mshambuliaji huyo wa Hispania alilazimika kutolewa nje katika mchezo waliofungwa kwa bao 1-0 nyumbani na Manchester City Jumamosi iliyopita.

Sasa kocha Antonio Conte yupo katika wakati mgumu baada ya kugundua tatizo hilo ni kubwa kuliko alivyotegemea.

Shirikisho la Soka la Hispania limethibisha hilo baada ya kumfanyia vipimo Morata na kubaini tatizo hilo la msuri.

Maumivu hayo yatamweka nje kwa mwezi wote wa Oktoba na nusu ya Novemba..

Conte sasa amebaki na mshambuliaji mmoja tu Mbelgiji  Michy Batshuayi kwa sasa ndiye mshambuliaji  anayetambuliwa kuziba pengo la Morata.