Mwakyembe apewa ujanja na Watanzania Afrika Kusini

Muktasari:

  • Wakizungumza na Waziri Mwakyembe aliyewasili jana nchini Lesotho, Watanzania hao wamedai kuwa kuna kundi kubwa la nyota wa Kitanzania nje ya nchi ambao wanaweza kuibeba Taifa Stars.

Watanzania waishio Afrika Kusini wamempa ushauri Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dokta Harrison Mwakyembe kuandaa utaratibu wa kuwapata nyota wengi Watanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Wakizungumza na Waziri Mwakyembe aliyewasili jana nchini Lesotho, Watanzania hao wamedai kuwa kuna kundi kubwa la nyota wa Kitanzania nje ya nchi ambao wanaweza kuibeba Taifa Stars.

Wamedai kuwa ukiwekwa utaratibu mzuri, nyota hao watapatikana kwa wingi na kuwa chachu ya Stars kupiga hatua.

Walitolea mfano wa mchezaji Hassan Sembi ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa Ureno ingawa huwa haitwi kwenye timu ya Taifa