Liverpool yatupwa kwa Man City Ligi ya Mabingwa

Muktasari:

  • Droo hatua ya robo fainali yapagwa huku miamba wa soka wa England wakikutanishwa

Timu ya Liverpool imejikuta ikiangukia mdomoni mwa Manchester City kwenye droo ya hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Droo hiyo iliyochezeshwa leo Ijumaa pia imezipanga pamoja Real Madrid na Juventus ambazo zimewahi kukutana hatua ya fainali mwaka 2017.

Timu zingine ambazo zitakutana kwenye robo fainali hiyo ni Barcelona ambayo imepangwa na As Roma. Pia Sevilla wameangukia kwa Bayern Munich.

Mchezo wa kwanza baina ya Man City na Liverpool utapigwa kwenye dimba la Anfield.