Pogba, Mourinho wanasiri nzito

Muktasari:

Wawili hao katika siku za karibuni wamepoteza maelewano

London, England. Kiungo Paul Pogba na Jose Mourinho bado wanategemea licha ya kiungo huyo kucheza kwa kiwango bora dhidi ya Bournemouth.

Kiungo huyo jana usiku alicheza soka maridadi katika mchezo ambao Manchester United ilishinda mabao 2-0 ugenini.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu England, Pogba alimiliki vyema eneo la kiungo kabla ya kutolewa dakika 80.

Baada ya kwenda katika benchi, kocha huyo Mreno alimpigia makofi kwa kazi nzuri, lakini hakumpa mkono.

Pogba awampa mkono nahodha aliyekuwa kwenye benchi la ufundi, Michael Carrick na msaidizi wa Mourinho, lakini hakumpa mkono bosi wake.

Kiungo nguli wa zamani wa timu hiyo, Paul Scholes alisifu kiwango bora cha kiungo huyo na alimtaka kuendeleza makali katika mechi zijazo.

Pogba na Mourinho wamekuwa na mzozo wa muda mrefu, huku kiungo huyo akitupiwa lawama kuhusu kiwango chake licha ya kununuliwa kwa bei mbaya Pauni89 milioni kutoka Juventus.