Mabaunsa wamzuia Mike Tyson uwanja wa ndege Chile

Friday November 10 2017

 

Mtandao wa Tmz umeweka picha zinazomuonyesha nyota wa zamani wa masumbwi na bingwa wa dunia, Mike Tyson akisindikizwa na askari wa uwanja wa ndege na kumtaka arejee Marekani.

Inadaiwa kuwa mamlaka husika nchini humo zimemzuia Tyson kwa kile kilichodaiwa kuwa hajakidhi vigezo vya kuingia Chile.

Jambo hilo limesababisha Tyson kukosa pesa nyingi kwa kuwa bondia huyo alikuwa anakwenda Chile kwa ajili ya kutengeneza tangazo.

Advertisement