Mapishi

Futari  Chapchap

Jaribu uji wa viazi vitamu ufurahie futari yako

Kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kinywaji aina ya uji kinatumika sana na imekuwa kawaida katika kipindi cha mfungo.

Kuna aina mbalimbali za uji, kwa ufupi wapo wanaokunywa wa unga wa sembe na maziwa, unga wa ulezi, unga  na wa unga wa muhogo.

Leo wafuatiliaji wa kolamu hii nitawaelekeza jinsi ya kupika uji wa viazi vitamu.


Mahitaji:

Viazi vitamu vikubwa viwili au kulingana na ukubwa wa familia.

Maziwa freshi (ya maji) kikombe kimoja  na nusu
Sukari nusu  kikombe
Iliki ya unga robo  kijiko cha chai
Karanga zilizosagwa kulingana na wingi wa viazi.

Jinsi ya kutayarisha
Chemsha viazi hadi viive vizuri.

Menya maganda kisha kiponde hadi kiwe laini kwa kutumia mwiko au kisage kwenye mashine (blenda)

Weka viazi vilivyosagwa  kwenye sufuria utakayotumia kupikia, weka maziwa, karanga na sukari kisha changanya vizuri hadi vichanganyike.

Punguza moto, weka iliki na koroga tena na uache uchemke kwa dakika 10 hadi 15 kwa moto mdogo sana  kisha uipue tayari kwa kunywewa.

 

 

 

 

Mchemsho wa samaki

Kwa kuwa futari huliwa na watu waliofunga inahitaji kuwe na kitoweo kidogo hivyo kutokana na changamoto ya muda, mchemsho wa samaki na mbogamboga unafaa.

Mahitaji

 Samaki wawili wakubwa kiasi

Karoti

 Pilipili hoho

Pilipili mbuzi (pilipili kali)

 Vitunguu maji

Chumvi

 Nyanya

 Ndimu

Jinsi ya kuandaa

Osha samaki vizuri.

Osha nyanya, hoho, kitunguu maji  na karoti kisha  katakata kila kimoja katika vipande vidogo.

Weka vitu vyote katika sufuria isipokuwa chumvi na pilipili mbuzi (pilipili kali).

 

Funika na acha vichemke kwa nusu saa. Kisha weka

chumvi na pilipili mbuzi, utaangalia maji yaliyomo kwenye mchemsho wako wa samaki kama yanatosha supu, kama hayatoshi ongeza kidogo, acha ichemke na itakuwa tayari kwa kuliwa.

 

Hizi ni futari tatu unazoweza kuzipika kwa haraka ukiwa na saa moja na nusu zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Muhimu: Siyo vibaya ukitumia majiko mawili ili kuokoa muda.