VIDEO: Mashabiki waonja utamu wa Bendi ya Bogoss laivu

Muktasari:

  • Wapo waliosema, Nyoshi isiwe nguvu ya soda,watu waliojaa hapa sababu tu hawajamuona mwaka mnzima akiwa stejini,hivyo hatakiwi kuachia nafasi aliyoaanza nao.

Mashabiki waliohudruria katika uzinduzi huo wa Bendi ya Bogoss jana Jumamosi, baadhi walizungumza na MCL Digital na kusema kuwa,ujio wa Nyoshi na Bendi yake ya Bogoss ni mzuri,ila isije akabweteka akarudi nyuma kwani moto aliouanza uendelee kuwaka.

Wapo waliosema, Nyoshi isiwe nguvu ya soda,watu waliojaa hapa sababu tu hawajamuona mwaka mnzima akiwa stejini,hivyo hatakiwi kuachia nafasi aliyoaanza nao.

Katika uzinduzi huo,baadhi ya wasanii waliohudhuria ni Mkurugenzi wa bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) Asha Baraka, Rich One, Dudu Baya, Jose Mara, Mwanamuziki 33 aliyekuwa FM Academia na wengine wengi.

Ujio wa Bendi hiyo mpya inatarajiwa kuleta hamasa katika muziki wa danis nchini ambapo kwa muda mrefu umeonekana kusuasua.

Bendi hiyo kwa sasa inatajwa kuwa bedni yenye wanamuziki wengi vijana chipukizi ambapo Rais wao aliwahi kunukuliwa kwamba lengo lake kuwa na vijana wengi ni kuwaandaa kuwa waimbajiwazuri hapo baadaye hata atakapostaafu muziki.