P-Square: Ni ngumu kuandaa albamu bila mama

Muktasari:

Wasanii maarufu Barani Afrika na Dunia kwa ujumla,Peter na Paul Okye wanaounda kundi la  P-Square ,wamesema kuwa kinachowafanya wachukue muda kundaa albamu ni kukosekana kwa sapoti ya mama yao ambaye alifariki dunia Julai 13 mwaka jana.

Mapacha hao wamesema kuwa kabla mama yao hajafariki Dunia alikuwa pamoja nao studio walipokuwa watengeneza albamu na alikuwa akiwaombea wiki nzima kabla ya kuingiza albamu sokoni na hawajui kwa sasa itakuwaje.

“Alipokuwa hai alikuwa ni sehemu ya mafanikio yetu hasa kipindi ambacho tunaandaa albamu alikuwa akikesha nasi studio na kuombea hata kazi zetu lakini sasa maisha yamekuwa magumu na sijui tutafanyaje albamu tutakapokuwa tayari kuifanya”walilalamika wasanii hao.

Akifafanua zaidi Peter alisema kuwa mama yao alikuwa ni muumini mzuri na alikuwa na kanisa lake ambalo walishirikiana kulijenga tunachofanya kumuenzi ni kuhakikisha linaendelea.