Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Balozi wa EU nchini aitwa Ubelgiji

Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Roeland van de Geer.

Muktasari:

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Ulaya anaondoka leo usiku kwenda kwa ajili ya mashauriano na mabosi wake

Dar es Salaam. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Roeland van de Geer anaondoka nchini usiku wa leo baada ya kuitwa katika makao makuu ya umoja huo Brussels, Ubelgiji kujadili masuala ya kisiasa ya hivi karibuni nchini.
“Balozi Roeland ameitwa makao makuu Brussels kwa majadiliano na ngazi za juu za kisiasa wiki ijayo kuhusu matukio ya hivi karibuni,” alisema Balozi msaidizi, Charles Stuart alipoulizwa na gazeti hili Alhamisi.
Taarifa kutoka ubalozi huo zimeeleza kuwa balozi huyo alitarajiwa kuondoka nchini saa 5:55 usiku.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo kwa simu juzi usiku, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga hakuwa tayari kulizungumzia akisema atalitolea taarifa baadaye.
“Ndio nimefika kutoka ng’ambo, ni suala lenye utata ambalo kwanza nataka nijiridhishe na wenzangu wizarani. Tuzungumze hilo kesho (jana),” alisema Dk Mahiga.
Hata hivyo, jitihada za kumpata jana kama alivyoahidi hazikufanikiwa, kwani simu yake ilikuwa ikiita bila kupokewa wala kujibu ujumbe wa simu.
Licha ya kutokuwepo kwa maelezo rasmi ya Serikali kuhusu suala hilo, Stuart hakutaka kueleza kitakachozungumzwa na uongozi wa juu wa umoja huo kuhusu Tanzania.
Balozi Roeland anatarajiwa kukutana na mabosi wake Jumatatu.
Akizungumzia hatua ya balozi huyo kuitwa, Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia (CFR), Innocent Shoo alisema kunaweza kuhusishwa na masuala ya kisheria.
Balozi Roeland atakuwa wa pili kuondoka Tanzania katika mazingira hayo kwenye miaka ya hivi karibuni baada ya Awa Dabo, wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) aliyeondoka Aprili 2017.
Hata hivyo, Serikali ilisema Dabo aliondolewa kutokana na mzozo na wafanyakazi wenzake wa UNDP.