JPM ateua makatibu tawala Mara, Rukwa

Muktasari:

Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.

Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli leo tarehe  Septemba 9, 2016 amemteua  Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.

Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.

Pia, Rais Magufuli amemteua Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi naSymthies Emmanuel Pangisa ambaye pia amestaafu.

Tarehe ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye.