Sh16 trilioni kujenga reli ya kati

Muktasari:

Makubaliano hayo yalifanywa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servaciaus Likwelile kwa niaba ya Serikali na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China, Zhu Ying.

Dar es Salaam. Serikali imetiliana saini na Benki ya Exim ya China makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge).

Makubaliano hayo yalifanywa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servaciaus Likwelile kwa niaba ya Serikali na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China, Zhu Ying.

Zaidi ya Sh16 trilioni zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi huo wenye urefu wa kilomita 2,190.

Dk Likwelile alisema hatua hiyo inawezesha kazi ya upembuzi yakinifu, usanifu na uundwaji wa timu za pamoja kuanza kuanisha mahitaji halisi ya ujenzi wa mradi huo.