Vyeti homa mpya kwa watumishi

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako .

Muktasari:

Tofauti na siku za nyuma kulipokuwa na matangazo ya aina tofauti, magazeti ya juzi yalikuwa na utitiri wa matangazo ya watu kupotelewa na vyeti.

Dar es Salaam. Wakati taasisi na idara za Serikali zikiendelea kuhakiki vyeti kubaini watumishi wasiokuwa na sifa, watu wengi wamejitokeza kutangaza magazetini kupotelewa na vyeti vyao.

Tofauti na siku za nyuma kulipokuwa na matangazo ya aina tofauti, magazeti ya juzi yalikuwa na utitiri wa matangazo ya watu kupotelewa na vyeti.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema juzi kuwa Serikali itafanya uhakiki wa vyeti katika vyuo na sehemu za kazi.

Juzi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Godius Kahyarara alitoa waraka akisema wafanyakazi watakaoshindwa kuwasilisha vyeti vyao halisi hawatalipwa mishahara.