Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanesco Dom yaonja ukaribu wa viongozi

Muktasari:

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana akiwa kwenye ukaguzi wa maeneo ya kutolea huduma za jamii, ikiwa ni maandalizi ya Serikali kuhamia hapa, aliagizaTanesco kupeleka nishati hiyo maeneo yanayovutia wawekezaji.

Dodoma. Mara nyingi watendaji wa mikoani hujisahau kwa utendaji tofauti na Dar es Salaam ambako viongozi wakuu wa nchi hupatikana, hali hiyo imeanza kubadilisha kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Dodoma baada ya Serikali kuanza kuhamia.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana akiwa kwenye ukaguzi wa maeneo ya kutolea huduma za jamii, ikiwa ni maandalizi ya Serikali kuhamia hapa, aliagizaTanesco kupeleka nishati hiyo maeneo yanayovutia wawekezaji.

Pia, alisema Serikali itaanza mchakato wa kutoza kodi unga wa jasi (gypsum) unaoingizwa nchini ili kulinda viwanda vya ndani.

 “Pelekeni umeme katika maeneo ambayo hayana huduma, ili wawekezaji wakute maji na umeme upo,” alisema Majaliwa.

Awali, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu alisema wameanza maandalizi ya ujenzi wa njia mpya ya umeme itakayoongeza upatikanaji wa nishati hiyo.