Wizara ya Afya yatangaza nafasi 3152 za ajira

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Muktasari:

Miongoni mwa nafasi hizo za ajira hizo ni pamoja na wauguzi, daraja la kwanza na la pili, wataalamu wa maabara na wengineo.

Dar es Salaam. Wizara ya Afya, imetangaza nafasi za ajira   3152 kwa wahitimu katika kada mbalimbali za afya nchini.

Taarifa iliyotolewa jana na kuwekwa kwenye ukurasa wa Twitter wa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu imeeleza kuwa, wizara ina jukumu la kuwapangia vituo waombaji wenye sifa kwa mujibu wa waraka wa maendeleo ya utumishi wa umma.

Miongoni mwa nafasi hizo, zipo za wauguzi daraja la kwanza na la pili, wapo wataalamu wa maabara, wanateknolojia na wataalamu wa lishe.