Airtel yazindua bando la HATUPIMI dakika zenu za muda wa maongezi

Mkurugenzi wa Masoko, Isack Nchunda

Muktasari:

  • “Airtel HATUPIMI bando” itapatikana katika  vifurushi mbalimbali ikiwemo kifurushi cha  siku, wiki na mwezi  vilivyosheheni  dakika zisiso na kikomo zinazowawezesha wateja wa Airtel kuongea na kufanya mengi zaidi bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa muda wa maongezi kwa kuwa hakuna kupimiwa dakika za maongezi.

Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua OFA kabambe  ijulikanayo kama HATUPIMI bando  itakayowawezesha wateja wake wote nchini kuongea bila kikomo mara tu baada ya kujiunga.

“Airtel HATUPIMI bando” itapatikana katika  vifurushi mbalimbali ikiwemo kifurushi cha  siku, wiki na mwezi  vilivyosheheni  dakika zisiso na kikomo zinazowawezesha wateja wa Airtel kuongea na kufanya mengi zaidi bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa muda wa maongezi kwa kuwa hakuna kupimiwa dakika za maongezi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa hii kabambe,  Mkurugenzi wa Masoko, Isack Nchunda alisema “ Airtel Hatupimi, sasa Hatupimi dakika zenu za maongezi, tunaleta huduma hizi nafuu kwa kuwa tunaamini katika kuendelea kuboresha huduma zetu  ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa  kuwapatia thamani ya pesa zao katika huduma na bidhaa zetu."