Akamatwa kwa kujiunganishia bomba la mafuta nyumbani kwake
Muktasari:
Samwel anashikiliwa kwa tuhuma za kutoboa na kujiunganishia bomba la mafuta la TPA
Dar es Salaam. Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakishirikiana na Jeshi la Polisi wanamshikilia Samwel Kilang'ani(63) kwa tuhuma ya kutoboa bomba la mafuta ya dizeli mali ya TPA na kujiunganishia hadi kwenye nyumba yake ambako ameweka mantanki makubwa ambayo ameyachimbia chini.
Msemaji wa TPA, Janeth Ruzangi amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo huku polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ikiendelea kumshikilia kwa uchunguzi zaidi.