Rais Magufuli afanya mabadiliko haya baraza la mawaziri

Muktasari:

Wizara hizo zimeongezeka kutokana na wizara mbili kugawanywa huku nafasi za manaibu wapya zikiwa tano

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametangaza baraza jipya la mawaziri lililoongezeka kutoka wizara 19 hadi 21.

 

Wizara hizo zimeongezeka kutokana na wizara mbili kugawanywa huku nafasi za manaibu wapya zikiwa tano.

 

Akitangaza leo Jumamosi baraza hili jipya, Rais Magufuli amesema Wizara ya Nishati na Madini imegawanywa mara mbili, sasa kutakuwa na Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini.

 

Amesema hatua hiyo inatokana na umuhimu wa rasilimali hiyo kwa taifa na kwamba wizara hizo zote kila moja itakuwa na waziri na naibu wake.

 

Rais Magufuli ametaja mabadiliko mengine katika Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambayo kwa sasa kutakuwa na Wizara ya Kilimo inayojitegemea na nyingine itakuwa ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

 

Amesema sababu za kufanya mabadiliko hayo ni kutokana na umuhimu wa sekta hiyo inayoajiri asilimia 75 ya Watanzania nchini hivyo ni vyema ijitegemee. Kila wizara itakuwa na waziri na naibu wake.

 

Mabadiliko mengine ni katika wizara ya Tamisemi baada ya kuweka nafasi mbili za manaibu waziri kwa sababu ni wizara inayogusa sehemu kubwa ya wananchi.

 

 

Baraza la Mawaziri

 

Wizara ya Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika

 

Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi

Mawaziri - Suleiman Jafo, manaibu waziri - Josephat Kandege na Joseph George Kakunda.

 

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Waziri - January Makamba, Naibu Waziri, Kangi Lugola.

 

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu Waziri - Jenista Mhagama, manaibu Stella Ikupa na Anthony Mavunde.

 

Wizara ya Kilimo ni Dk Charles Tzeba na naibu wake Dk Mary Mwanjelwa.

 

Wizara wa Mifugo na Uvuvi ni Luhaga Mpina na naibu wake ni Abdallah Ulega

 

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na manaibu wake Atashasta Nditiye na Elias Kwandikwa.

 

Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango na naibu waziri ni Ashantu Kijaji.

 

Wizara ya Nishati ni Dk Medard Kalemani na naibu wake ni Subira Mgalu.

 

Wizara wa Madini ni Angellah Kairuki na naibu wake Haruni Nyongo.

 

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi

 

Wizara wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustino Mahiga na naibu Dk Susan Kolimba.

 

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi

 

Wizara ya Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na naibu wake Hamad Masauni.

 

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na naibu ni Angelina Mabula.

 

Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala na naibu wake ni Ngailonga Hasonga.

 

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na naibu wake ni Stella Manyanya.

 

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako na naibu wake ni  Wiliam Ole Nasha.

 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu na  naibu wake ni Dk Faustine Ndugulile. 

 

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na naibu wake ni Juliana Shonza.

 

Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwele na naibu wake ni Juma Aweso.