Bodi ya filamu yakanusha kuzuia filamu za kigeni

Dar es Salaam. Bodi ya Filamu Tanzania, imekanusha taarifa zilizosambaa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa Serikali inazuia kwa makusudi uingizaji,usambazaji na uuzwaji wa filamu za kigeni nchini.

Madai ya taarifa hiyo ni kwamba Serikali ina lengo la kuwalazimisha wananchi kuangalia filamu za ndani (bongo movie).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na bodi hiyo leo zinaeleza kuwa habari hiyo haina ukweli wowote na umma wa Tanzania una tahadhalishwa kuipuuzia .

“Taarifa hizi zina lengo la kupotosha na kudhoofisha juhudi za Serikali za kuhakikisha kila mtu anafanya biashara ya filamu kwa kufuata sheria na kanuni zilizopo,”imeeleza taarifa hiyo.