Chadema waanza mbinu za 2020

Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga .

Muktasari:

Akifungua mafunzo kwa viongozi wa Baraza la Uongozi la Chadema Mkoa wa Pwani, Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga alisema ruzuku haiwezi kuendesha chama na kwamba, fedha hizo zisiwagombanishe wanachama na viongozi wao.

Morogoro. Wanachama wa Chadema wametakiwa kutotegemea ruzuku wanayopata, badala yake watumie rasilimali zao kukijenga chama kuhakikisha kinapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu 2020.

Akifungua mafunzo kwa viongozi wa Baraza la Uongozi la Chadema Mkoa wa Pwani, Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga alisema ruzuku haiwezi kuendesha chama na kwamba, fedha hizo zisiwagombanishe wanachama na viongozi wao.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Jimbo la Chalinze mkoani Pwani, Mathayo Torongey alisema mafunzo hayo yamelenga kuing’oa CCM ambayo Mkoa wa Pwani imeonekana kuwa ni ngome yake.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa chama hicho Mkoa wa Pwani, Said Mazoea aliwataka wanachama kukitumikia chama hicho kwa uadilifu na uaminifu na kuwaonya baadhi yao ambao wamekuwa wakitumiwa na CCM.