Mwenyekiti Chadema wilaya ya Karatu afariki dunia

Marehemu Moshi Darabe mwenyekiti chadema wilaya  Karatu

Muktasari:

Kwa mujibu wa mbunge wa viti maalum wa chama hicho, Cesilia Parreso amesema Darabe ambaye pia ni diwani wa kata ya Baray, amefariki  jana  na anatarajiwa kuzikwa kesho.

Karatu. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha, Moshi Darabe amefariki dunia.

Kwa mujibu wa mbunge wa viti maalum wa chama hicho, Cesilia Parreso amesema Darabe ambaye pia ni diwani wa kata ya Baray, amefariki  jana  na anatarajiwa kuzikwa kesho.

“Atazikwa kesho baada ya kuagwa katika uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu.  Alikuwa anasumbuliwa na sukari na alifariki akiwa anapelekwa hospitali ,” amesema Parreso.

Darabe amekuwa mwenyekiti wa Chadema tangu mwaka 2003 na alikuwa diwani kuanzia mwaka 2000.