Wednesday, January 11, 2017

Diamond kutumbuiza kwenye mashindano ya AFCON

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye akimkabidhi Bendera mwanamuziki Diamond Platnumz kwa ajili ya kwenda kutumbuiza katika tuzo za AFCON nchini Gabon. Anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania, Salum Salum na balozi wa DSTV Lucas Mhavile maarufu Joti. 

By Harrieth Makwetta mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo na Kampuni ya DSTV zimefanikisha safari ya mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz ya  onyesho lake katika ufunguzi wa mashindano ya AFCON nchini Gabon.

Diamond ni miongoni mwa wasanii teule watakaotumbuiza katika hafla hiyo.

Akizungumza wakati akimkabidhi bendera ya Tanzania, Waziri wa Wasanii, Nape Nnauye amesema Tanzania imepata nafasi ya pekee kupata mshiriki kupitia sanaa ya muziki.

"Hii inaonyesha namna sanaa yetu inavyozidi kukua siku hata siku, Diamond amekuwa miongoni mwa wasanii watatu Afrika watakaotumbuiza live wimbo maalum katika mashindano haya, ambao pia utatumika katika mashindano hayo," amesema Nape.

-->