Dk Nyantahe awa mwenyekiti NDC

Dk. Samuel Nyantahe

Muktasari:

Rais wa John Magufuli amemteua Dk  Nyantahe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Dar es Salaam. Rais wa John Magufuli amemteua Dk. Samuel Nyantahe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza leo kuwa uteuzi huo umeanza  Julai 20, 2016.

Kabla ya uteuzi huo, Dk  Nyantahe alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

Dk Nyantahe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Chrisant Mzindakaya ambaye amejiuzulu