Gwajima kuwavua mataulo wanaomchokoza

Muktasari:

Akihubiri leo, Gwajima amesema wakiendelea atawavua mataulo ili jamii iwaone.

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewatahadharisha wanaomchokoza akisema ni sawa na mtu anayeanzisha ugomvi huku akiwa amevaa taulo.

Akihubiri leo, Gwajima amesema wakiendelea atawavua mataulo ili jamii iwaone.

Bila kufafanua kuhusu kauli hiyo, Gwajima amesema hawezi kunyamaza wakati watu wanaendelea kumfuata fuata.

"Leo nitakwapua mataulo ya   watu,"amesema huku akishangiliwa na waumini wake.