JPM: Bado ndege mbili kubwa zinakuja

Rais John Magufuli

Muktasari:

Ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa ndege mbili aina ya Bombardier Q 400 unaofanyika sasa katika uwanja wa JNIA.

Rais John Magufuli amesema licha ya mengi kuzungumzwa kuhusu ndege hizo lakini  bado serikali itaendelea kununua ndege nyingine kubwa mbili moja yenye uwezo wa kubeba abiria 160 na nyingine abiria 240.

Ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa ndege mbili aina ya Bombardier Q 400 unaofanyika sasa katika uwanja wa JNIA.

“Mengi yamezungumzwa kuhusu ndege hizi mpaka unajiuliza nimekosea nini kununua ndege hizi. Wapo waliosema zina mwendo mdogo kama bajaji, lakini imetoka Canada hadi Dar, bajaji ingetumia siku ngapi?” alihoji Rais