Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KLM kugharamia safari ya kurudi ya wanafunzi wa Lucky Vincent

Muktasari:

Gharama ya ndege ya DC 8 iliyotumika kuwasafirisha majeruhi watatu wa Lucky Vincent pamoja na wasindikizaji wao, kama ingelipwa ingekuwa ni dola za Marekani 400,000 ambazo ni zaidi ya zaidi ya Sh800 milioni.

Arusha. Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent ya jijini hapa waliosafirishwa nchini Marekani kwa ajili ya matibabu, watarejea nchini pamoja na waliowasindikiza kwa usafiri wa bure uliotolewa na Shirika la Ndege la Uholanzi(KLM)

Wanafunzi waliosafirishwa ni Sadia Awadh,Wilson Tarimo na Doreen Elibarick kila mmoja akiwa na mama yake, muuguzi na daktari bingwa wa mifupa ambao waliondoka nchini tangu Mei 14, mwaka huu

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyewezesha safari ya kwenda Marekani kupitia taasisi Stemm ambayo ni mwenyekiti mwenza, amesema kuwa usafiri huo uko tayari muda wowote matibabu ya wanafunzi hao yatakapokuwa yamekamilika.

"Napenda kuthibitishia kuwa usafiri wa kurudi upo jambo la muhimu Watanzania wote tumwombe Mungu wapate nafuu kwa haraka baada ya upasuaji waliofanyiwa ili waweze kuendelea na masomo yao,"amesema Nyalandu.