Kesi ya ubunge wa Longido bado mbichi

Muktasari:

Lengo la kusogeza mbele ni  kuwajumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Msimamizi wa Uchaguzi.

Arusha. Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imesogeza mbela kusikiliza hukumu ya rufani ya kesi ya ubunge wa Longido.

Lengo la kusogeza mbele ni  kuwajumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Msimamizi wa Uchaguzi.

Majaji wa Mahakama ya Rufani, Sauda Mjasiri, Mussa Kipenka na Profesa Ibrahim Juma wametoa uamuzi huo jana uliosomwa na Msajili wa Mahakama, John Kahyoza.

Katika maamuzi hayo, aliyekuwa Mbunge wa Longido (Chadema), Onesmo ole Nangole anayepinga matokeo kutenguliwa, alitakiwa kuwaongeza ndani ya siku 21, AG na Msimamizi wa Uchaguzi kwa kuwa ni muhimu katika kesi hiyo ili kuendelea na rufani ya msingi.