Fanny Zanzibar atoboa sababu ya kurudia ‘Madam Hero’

Muktasari:

Aliyeurudia wimbo Madam Hero wa Hamisa Mobetto, Khalfan Ali Rashid maarufu’Fany Zanzibar’ anasema pamoja na kwamba tayari alishatoa nyimbo zake tatu ikiwemo Nimerogwa, Tukikutana, I love you, wimbo huo unakuwa wa nne kwake.

Kwa nini hakuamua kurudia nyimbo za wasanii wengine hususani wakongwe kama ambavyo wasanii wengine wamekuwa wakifanya, ‘Fany Zanzibar’ anasema ni kutokana na wimbo huo kubeba ujumbe mzito wa kuelimisha jamii na ndio maana akaamua.

Funny aliyezaliwa mwaka 1994 katika hospitali ya Mnazimoja visiwani Zanzibar, anasema kipaji chake cha kuimba kilianzia akiwa shule ambapo alikuwa mtunzi wa tenzi mbalimbali huku mwanamuziki aliyemvutia zaidi hadi kuingia katika fani hiyo muzikiaki akiwa ni Alikiba

Pia anasema pamoja na kwamba hajawahi kuonana na Hamisa ana kwa ana anatamani siku moja wakutane na ikiwezekana kuweza kufanya naye kazi japokuwa anasema kuwa kitendo cha Hamisa kuuweka wimbo wake kwenye Instagram yake, ni dalili njema kwake za kuelekea huko.

Wasanii wengine ambao anapenda siku moja angefanya nao kazi ni pamoja na Diamond, Jux, Gigy Money na kudai kwamba baadhi yao ameshaanza kuwasiliana nao.