Kubenea matatani tena
File Photo
Muktasari:
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri, Wakili wa Serikali, Dereck Mukabatunzi alidai jana kuwa Kubenea (46) alifanya kosa hilo Julai 25, Mtaa wa Kasaba wilayani Kinondoni.
Dar es Salaam. Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shtaka la kutangaza habari za uongo ambazo zingeweza kusababisha hofu kwa jamii.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri, Wakili wa Serikali, Dereck Mukabatunzi alidai jana kuwa Kubenea (46) alifanya kosa hilo Julai 25, Mtaa wa Kasaba wilayani Kinondoni.
Mukabatunzi alidai Kubenea (pichani) alisambaza habari ya uongo kwenye gazeti la Mwanahalisi la Julai 25 hadi 31 toleo namba 349 ISSN 1821-5432 ikiwa na kichwa cha habari ‘Yuko wapi atakayeiyokoa Zanzibar’. Alidai habari au makala hiyo ingeweza kusababisha hofu kwa jamii au kuharibu hali ya amani.
Kubenea alikana kosa hilo. Upande wa mashtaka ulidai upelelezi umekamilika na ukaomba kesi ipangiwe tarehe kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.