Lissu apeleka maombi ya dhamana Mahakama Kuu

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Muktasari:

Wamefikia hatua hiyo, baada ya Jeshi la  Polisi linalomshikilia kumnyima dhamana.

Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kupitia Wakili wake Peter Kibatala wamepeleka maombi Mahakama Kuu  kuomba apewe dhamana.

Wamefikia hatua hiyo, baada ya Jeshi la  Polisi linalomshikilia kumnyima dhamana.

Akizungumzia sakata hilo leo, Wakili Kibatala alisema polisi hawana sababu ya kuendelea kukaa na Lissu bila ya kumpa dhamana.

"Kosa analodaiwa kulifanya lilifanyika Januari 4, 2017 hadi Februari 6, 2017 ni mwezi,  kama ni muda wa kuchunguza kosa hata hati ya mashtaka ingekuwa tayari," amesema  Kibatala.