Lukuvi aombwa kurejesha ekari 20,000 kwa wananchi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi 

Muktasari:

Wakazi wa vijiji hivyo wamemuomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kubatilisha miliki ya ardhi hiyo.

Morogoro. Wananchi wa vijiji vya Kiwege na Mlilingwa wilayani Morogoro wameomba kurejeshewa zaidi ya ekari 20,000 walizozitoa kwa wawekezaji ambao wameshindwa kuziendeleza.

Wakazi wa vijiji hivyo wamemuomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kubatilisha miliki ya ardhi hiyo.

Wakizungumza na wataalamu kutoka Mtandao wa Jamii wa Uhifadhi wa Misitu Tanzania (Mjumita), wananchi hao walisema kuna mashamba mengi yametolewa kwa wawekezaji wakiwamo wafugaji lakini hayajaendelezwa.