Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makamu wa rais mgeni rasmi tuzo za bidhaa bora

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Muktasari:

Uzinduzi huo unafanyika Septemba 20 kwenye ukumbi wa Mlimani City, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  na Waziri wa Viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage na viongozi wengine mbalimbali wanatarajiwa kuudhuria kwenye hafla hiyo.

Dar es Salaam. Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wanatarajia kuzindua kampuni ya fahari ya Tanzania ambayo itakwenda sanjari na utoaji wa tuzo wa bidhaa 50 bora zinazozalishwa nchini.
Uzinduzi huo unafanyika Septemba 20 kwenye ukumbi wa Mlimani City, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  na Waziri wa Viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage na viongozi wengine mbalimbali wanatarajiwa kuudhuria kwenye hafla hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Mkurugenzi wa tspf Godfrey Simbeye amesema kampuni hiyo ina malengo manne, ikiwamo kuhamasisha uzalishaji wa viwango bora ili kukidhi matakwa ya soko, wazalishaji kuongeza thamani ya bidhaa au kuzalisha kwa kutumia malighafi za kitanzania na kuongeza ushindani wa kuuza bidhaa kwenye soko la nje.