Vigogo Chadema waanza kuwasili Polisi

Muktasari:

Viongozi hao walisomewa mashtaka yakiwamo ya uchochezi, uasi na kuhamasisha maandamano.


Dar es Salaam.  Vigogo watatu wa Chadema, wamewasili katika Kituo Kikuu cha Polisi, jijini Dar es Salaam, leo Aprili 13, wanakotakiwa kuripoti kila Ijumaa kama Mahakama ilivyowataka.

Walioonekana kituoni hapo mpaka sasa ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya na Naibu Katibu Mkuu Visiwani, Salum Mwalimu.

 Viongozi hao waliamriwa kuripoti polisi kila Ijumaa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kusomewa mashtaka mbalimbali ikiwamo ya uchochezi, kuhamasisha maandamano na kutotii amri ya kuacha kuandamana.

 Mcl Digital itaendelea kukujuza yanayojiri kituoni hapo.