Mgodi Mwadui wasababisha vilio

Mgodi wa Williamson Petra Diamond Ltd mkoa wa  Shinyanga

Muktasari:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne alisema wafanyakazi waliokufa kwenye tukio lilitokea wakati wakirekebisha mashine.

Shinyanga. Kuanguka kwa mtambo baada ya Kamba iliyokuwa imeushikilia kukatika katiak Mgodi wa Williamson Petra Diamond Ltd mkoani Shinyanga, kumesbabisha vilio na simanzi kwa wafanyakazi na familia zao.

Wafanyakazi waliokufa kwa kuangukiwa na mtambo huo ni Benjamin Zephania (29) na Alex Mashenene (32) wote wakazi wa Mwadui, wilayani Kishapu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne alisema wafanyakazi waliokufa kwenye tukio lilitokea wakati wakirekebisha mashine.

Muliro alisema wafanyakazi hao walikuwa mafundi wa mgodi na kwamba, mtambo ulianguka baada ya kamba iliyokuwa imeushikilia kukatika.