‘Kama Manula tungepigwa 10’

Muktasari:

  • Katika mchezo huo wa mwisho wa hatua ya makundi ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika 2017, bao hilo pekee la Nigeria lilifungwa na mshambuliji Kelechi Iheanacho dakika ya 78 kwenye Uwanja wa Uyo, Akwa Ibom.

Dar es Salaam. Nyota wa zamani wa Yanga na Tanzania, Kitwana Manara amesema kama si umakini wa kipa Aishi Manula, Taifa Stars ingeweza kufungwa hata mabao 10-0 kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Nigeria.

Katika mchezo huo wa mwisho wa hatua ya makundi ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika 2017, bao hilo pekee la Nigeria lilifungwa na mshambuliji Kelechi Iheanacho dakika ya 78 kwenye Uwanja wa Uyo, Akwa Ibom.

Manula alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya Nigeria ambayo safu yake ya ushambuliaji iliundwa na mastaa wanaotamba kwenye Ligi Kuu England.

Uimara wa Manula katika kuokoa mashambulizi ya Nigeria ulionekana kwenye dakika ya 2, 12, 24, 28, 58 na 60 alipowanyima mabao ya wazi washambuliaji, Ahmed Musa, Odion Ighalo, John Obi Mikel, Victor Moses na Iheanacho.