Ribery ashukuru Pep kuondoka Bayern

Franck Ribery

Muktasari:

Ribery amesema kuwa sababu ya kusema hivyo ni kwa kuwa kocha huyo hakuwa akimwaamini.

MUNICH, UJERUMANI. WINGA Franck Ribery wa Bayern Munich amesema kitendo cha kocha kwa Pep Guardiola kuhamia Manchester City kwake ni jambo zuri.

Ribery amesema kuwa sababu ya kusema hivyo ni kwa kuwa kocha huyo hakuwa akimwaamini.

Ribery akiwa chini ya Pep, alianza mechi sita tu za Ligi Kuu Ujerumani maarufu Bundesliga msimu uliopita na hivyo sasa amefarijika baada ya kocha huyo kuondoka.

Anaamini hatua ya kocha huyo kuondoka inamfungulia mwanzo mpya wa kujenga jina lake ambalo chini ya kocha huyo Mhispaniola lilianza kufifia baada ya kusugulishwa benchi.

Ribery anaamini chini ya kocha mpya wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti mambo yatakuwa mazuri.